Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema akiri bangi kukutwa kwake

Thu, 21 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu amekiri mahakamani kuwa msokoto unaodhaniwa kuwa ni bangi ulikutwa nyumbani kwake.

Hata hivyo, alisema hajui ni wa nani kwa sababu nyumbani kwake wanaingia watu mbalimbali kwa kuwa yeye ni msanii.

Wema alisema hayo jana mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi inayomkabili ya kukutwa na dawa za kulevya.

Akiongozwa na wakili wake, Albert Msando, Wema ambaye pia aliwahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2006, alisema misokoto hiyo ilikutwa katika chumba cha kuhifadhia nguo, pochi na viatu.

“Ulikutwa kwenye chumba wanacholala wanamuziki wawili, Jordan na Miraji,” alisema Wema wakati akijitetea na wafanyakazi wake, Angelina Msigwa (23) na Matrida Abas (19).

Alibainisha kuwa nyumbani kwake walikuwa wanaishi yeye, wafanyakazi wake wawili, wadogo zake wawili, Agray Philemon na Fanuel Evalast na vijana wawilï wanamuziki, Miraji na Jordan.

Alidai Februari 3, 2017 alitakiwa kuripoti polisi kati ya saa tano asubuhi kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. “Siku hiyo tulifika polisi saa tano asubuhi na wenzangu watano tukasubiri hadi saa 10 jioni, ulipofika muda huo alifika Makonda na kutuita mmoja mmoja, katika chumba, alikuwapo na Afande (Simon) Sirro,” alieleza Wema.

Alidai kuwa wakiwa humo aliulizwa kama anatumia dawa za kulevya au kuuza na aliwajibu hapana.

Aliendelea kudai kuwa baada ya mahojiano hayo walipelekwa mahabusu ambako walikaa kwa siku saba na Februari 5 nyumba yake ilipekuliwa.

Hakimu Mkazi, Thomas Simba atatoa hukumu ya kesi hiyo Julai 16 mwaka huu.

Chanzo: mwananchi.co.tz