Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema aibuka tena na ishu ya kukosa mtoto

Wemaaa Wema aibuka tena na ishu ya kukosa mtoto

Sat, 18 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Filamu Bongo, Wema Sepetu anatamani sana kupata mtoto lakini hapati hivyo wakati mwingine hujifanya hataki.

Kupitia mahojiano yake na kituo cha redio Furaha TV Wema amesema kuwa mara nyingi mtu anaetaka kitu fulani huwa hapati kama yeye mara anatamani kupata ujauzito lakini hajawahi kupata kwa hiyo kuna kipindi anajifanya kama hataki anasema kabisa mbona sitaki ili itokee lakini moyoni anataka sana. ‘’Tunaotaka mimba ndio huwa hatupati wasiotaka wanapata.’’

Pia amesema kuwa “Baki single kama huwezi kumpa muda au kutenga muda kwa ajili ya mpenzi wako haina haja ya wewe kumpotezea muda mtoto wa watu dada au kaka anayetamani muda wako kama umekubali mpatie muda, huwezi fanya maisha yako hakuna atakayekulalamikia,” amesema Wema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live