Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema agoma kuchora tattoo ya Whozu

Wemaaa Wema Sepetu

Fri, 7 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu, amesema hawezi kuchora tattoo ya jina la mwanaume kwenye mwili wake kwa kuwa hakuna wa kumuamini zaidi ya baba yake mzazi.

Wema ameweka wazi kuwa mwanaume pekee aliyemchora kwenye mwili wake ni baba yake mzazi, marehemu Balozi Issac Sepetu.

"Hakuna kitu ambacho mwanaume anaweza kunifanyia cha ajabu kwake kiasi cha kumchora tattoo, hivyo siwezi kuchora jina la mwanaume yeyote kwenye mwili wangu zaidi ya wazazi au watoto wangu nikibarikiwa na si vinginevyo," amesema.

Hivi sasa Wema ana-date na Whozu, kabla ya ku-date na Whozu, Wema Sepetu ametoka na wanaume kadhaa, ifuatayo ni List ya wanaume maarufu ambao wema amewahi kutoka nao kimapenzi.

•T.I.D •Kanumba •Diamond Platnumz •Calisah •Idris Sultan •Chaz Baba •Ommy Dimpoz •Luis Munana •Danzak •Whozu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live