Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema aanika mbinu anayoitumia kuachana na wanaume

Wema Diamond Sg Wema aanika mbinu anayoitumia kuachana na wanaume

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Malkia wa sanaa ya filamu nchini, Wema Sepetu amesema kuwa mbinu kubwa ambayo huwa anaitumia kuwafukuza wanaume ambao hawapendi ni kuwaomba pesa kila siku jambo ambalo huwa linawafanya kukata tamaa na kuondoka kwenye maisha yake.

Wema amesema hayo wakati akihojiwa na chombo kimoja cha habari na kudai kuwa yeye ni masikini jeuri, hana tabia za kuomba pesa kwa mwanaume na anaamini mapenzi sio pesa bali ni upendo lakini yeye hufanya hivyo kwa mwanaume ambaye hamuhitaji.

“Mbinu ambayo huwa naitumia kuwafukuza wanaume ni invoice, si umejileta kwangu unanitaka nini? Nakupiga invoice moja baada ya nyingine kila siku ni matatizo tu, hapo ni sikupendi, yani ni invoice ambazo hazikakuki.

“Kwa sababu mimi sioni kwamba mapenzi ni kitu cha kuanza kupimana eti kwa sababu ni mpenzi wangu basi wewe unanipa tu pesa, kwa hiyo mapenzi yetu yanazunguka kwenye pesa tu?

“Lakini kama haupendi mapenzi ya pesa mimi huwa naona kama ni njia au namtafutia sababu ya kumfukuza ili kesho na keshokutwa asije tena.

“Kwa hiyo wadada tujitahidi, mimi ninaamini katika umasikini jeuri, sijui kwa nini lakini Mwenyezi Mungu kaniumba hivyo, siwezi kujishusha na kuanza kumuomba mwanaume pesa,” amesema Wema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live