Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema Sepetu mgonjwa, kesi yake yakwama

57333 Pic+wema

Tue, 14 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kesi ya kurekodi video ya ngono na kuisambaza katika mitandao ya kijamii inayomkabili mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu imekwama kuendelea ikielezwa kuwa mshtakiwa ni mgonjwa.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Mei 14, 2019 na wakili wa utetezi, Ruben Semwanza mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Maira Kasonde.

Semwanza amesema akiwa mahakamani hapo alipewa taarifa kuwa Wema anaumwa.

"Taarifa nimepewa asubuhi hii nikiwa hapa mahakamani na mdhamini wake hayupo amenieleza yupo kikazi mkoani Arusha, hivyo naiomba Mahakama hii ipange tarehe nyingine," amedai Semwanza.

Wakili wa Serikali, Grory Mwenda amedai kuwa shauri hilo lipo kwa ajili ya kusikilizwa pia shahidi aliyetakiwa awepo kutoa ushahidi naye hayupo hivyo aliiomba tarehe nyingine kwa ajili ya kusikilizwa.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Kasonde ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 11, 2019 itakaposikilizwa.

Pia Soma

Katika kesi hiyo, Wema anadaiwa Oktoba 15, 2018  katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam alirekodi video ya ngono na kuisambaza katika mtandao wake wa Instagram.

Chanzo: mwananchi.co.tz