Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema Sepetu azuiwa na walinzi kumuona Rais Samia

Wema Ashindwa Kutaja Umri Wake   VIDEO Wema Sepetu azuiwa na walinzi kumuona Rais Samia

Mon, 27 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji wa Bongo Movie kutoka Tanzania #WemaSepetu ameonesha kusikitishwa na suala la walinzi wa Ikulu kumzuia asiingie kwenye uzinduzi wa album mpya ya msanii Harmonize uliofanyika usiku wa kuamkia jana katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Staa huyo amesema kuwa, alifika ukumbini saa 3 usiku ambapo alivyofika getini alizuiliwa na walinzi hivyo alishindwa kuingia na ilimbidi akae na walinzi zaidi ya saa mbili.

Wema amedai kuwa alijisikia vibaya kwa kitendo hicho kwa sababu hakuweza kumsikia mama (Rais Samia Suluhu aliyekuwa mgeni rasmi) anaongea nini ila amemmiss kumuona live.

“Nimesikitika kwa sababu nimefika hapa saa tatu kasoro, mama tayari alikuwa yuko ndani, nimemmiss mama. Tumekaa hapa nje na walinzi kwa muda wa kama saa mbili lakini sijaweza kumpata mama ameongea nini kwa sababu nilikuwa nje.

“Nampenda mama na ninamuombea kwa Mungu amuepushe na mabaya, sisi kama wanae tunaendelea kumpa heshima na kumthamini kwa kile anachoyufanyia. Tunamshukuru na tutazidi kufurahi akiendelea kutimiza yale anayoahidi,” amesema Wema.

Siku moja kabla ya Tamasha hilo, Harmonize aliwakumbusha watu wote aliowaalika kuwa angependa wawahi kuingia ukumbini kwa sababu kutakuwa na mambo ya kiitifaki na Rais Samia akishaingia ukumbini, watu wengine hawataruhusiwa kuingia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live