Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema Sepetu azindua filamu, awatosa waandishi wa habari

Video Archive
Mon, 1 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Sherehe ya kuzaliwa malkia wa tuzo ya filamu za SZIFF mwaka 2018, Wema Sepetu iliingia doa baada ya kuwasotesha waandishi wengi nje kwa madai kuwa hawakuwa na haki ya kutoa habari hizo.

Sherehe hiyo iliyoendana sambamba na uzinduzi wa filamu yake mpya ilifanyika jana ukumbi wa Mlimani City na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali, mama yake mzazi, Miriam Sepetu na watu wengine maarufu.

 Baadhi ya viongozi waliokuwapo ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na  Katibu wa Bodi ya Filamu, Joyce Fisoo.

Kwa upande wa mastaa waliohudhuria ni ni Irene Uwoya, Jacob Steven’JB, Jenifer Kyaka, Faiza Ally, Rose Ndauka, Shamsa Ford, Mama Dangote, Esma Dangote, Juma Lokole na wengine wengi.

Hata hivyo kama ilivyozoeleka kwa waandishi kuchukua matukio, kwa mrembo huyo haikuwa hivyo na badala yake aliruhusu vyombo vichache huku wengi wao wakibaki nje mpaka saba za usiku kusubiria sherehe hiyo iishe.

Wakati wakiwa nje walitumia muda huo kuwanasa baadhi ya mastaa na kuwahoji mambo mbalimbali.

Baadhi ya waandishi waliozungumza na Mwananchi kwa masharti ya kutokutajwa jina walilaani kitendo hicho na kueleza kuwa ubaguzi huo hakupaswa kufanywa ikizingatiwa ni mtu ambaye amefanya kazi muda mrefu na wanahabari na anajua ni namna gani mashabiki na wapenda burudani wangependa kujua yaliyokuwa yakiendelea kwenye sherehe hizo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz