Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema Sepetu awatosa waandishi wa habari

20030 Pic+wema

Mon, 1 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

JUZI Ijumaa, Malkia wa tuzo ya filamu za SZIFF mwaka huu, Wema Sepetu alisheherekea miaka 30 ya kuzaliwa kwake huku akiwatosa kwa kiasi kikubwa Waandishi wa Wabari.

Sherehe hizo zilizoendana na uzinduzi wa filamu yake mpya, zilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali, mama yake mzazi, Miriam Sepetu na Mastaa kibao.

Baadhi ya viongozi waliokuwepo ni pamoja na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Katibu wa Bodi ya Filamu, Joyce Fisoo.

Wakati kwa upande wa mastaa wa Bongo Movie, alikuwepo Irene Uwoya, Jacob Steven’JB’, Jenifer Kyaka’ Odama na Shamsa Ford.

Wengine waliohudhuria ni Rose Ndauka, Faiza Ally, Duma, Petit Man, mama wa msanii Diamond alioongozana na mumewe na dada yake, Esma.

Hata hivyo, baadhi ya waandishi hawakuruhusiwa, jambo ambalo lilizaa maswali mengi kwa watu baada ya kuonekana wakipiga picha kambi nje huku wengine wakiondoka.

Chanzo: mwananchi.co.tz