Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema Sepetu atakiwa kutoweka picha za ngono mtandaoni

25029 WEMA+PIC TanzaniaWeb

Fri, 2 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtaka Miss Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu kutoweka video zinazohusiana na ngono wala maneno yoyote yenye mwelekeo huo katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Novemba Mosi, 2018 na hakimu mkazi, Maira Kasonde wakati akimpa masharti ya dhamana  Wema mara baada ya wakili wa Serikali, Mwanaamina  Kombakono kumsomea mlimbwende huyo shtaka linalomkabili.

Akipewa masharti ya dhamana, Wema ametakiwa kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya Sh10 milioni.

Kabla ya kupewa dhamana hiyo, Kombakono aliiomba mahakama kumpatia masharti magumu ya dhamana Wema ili iwe fundisho kwa wengine kwa kuwa ni msanii mwenye  wafuasi wengi wanaomuangalia hususan watoto.

Ruben Simwanza, wakili wa Wema aliomba mteja wake apewe dhamana ya masharti nafuu kwa kuwa ni haki yake.

Wema amesomewa shtaka moja la kuchapisha video ya ngono kupitia mtandao wake wa Instagram akidaiwa kufanya kosa hilo Oktoba 15, 2018 katika sehemu tofauti jijini Dar es Salaam.

Baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili, Hakimu Kasonde alimtaka Wema kuwa na mdhamini mmoja anayesaini bondi ya Sh10 milioni.

Wema alifanikiwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana na kuachiwa huru.

Shtaka linalomkabili Wema kwa mujibu wa sheria adhabu yake ni kulipa faini isiyopungua Sh20milioni ama kifungo kisichopungua miaka saba.

Chanzo: mwananchi.co.tz