Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema Sepetu aachiwa, akamatwa tena

65504 Wema+pic

Thu, 4 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu, lakini dakika chache baadaye askari wa Jeshi la Magereza walimkamata tena.

Mrembo huyo wa Tanzania mwaka 2006 aliyefika mahakamani hapo leo Alhamisi Julai 4, 2019 anakabiliwa na mashtaka ya kurekodi video ya ngono na kuisambaza katika mitandao ya kijamii.

Juni 24, 2019 mahakama hiyo ilimuonya Wema kutokukiuka masharti ya dhamana, vinginevyo haitasita kufutia dhamana yake.

Kauli hiyo ilitolewa na Hakimu Mwandamizi wa mahakama hiyo, Maira Kasonde wakati akitoa uamuzi kuhusiana na mshtakiwa kukiuka masharti ya dhamana.

Juni 17, 2019 Mahakama hiyo iliamuru mshtakiwa huyo kupelekwa rumande hadi Juni 24,  ili iweze kutoa uamuzi baada ya mshtakiwa huyo kujisalimisha mahakamani hapo.

Wema alijisalimisha mahakamani hapo Juni 17, 2019 baada ya Mahakama hiyo kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa huyo kutokana na kushindwa kufika mahakamani bila kutoa taarifa.

Pia Soma

Mahakama ya Kisutu, ilitoa hati ya kumkamata Wema, Juni 11, 2019 baada ya mshtakiwa huyo kuruka dhamana.

Wema ambaye alishawahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2006, anakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha video ya ngono na kusambaza katika mtandaoni  wa Istagramu kinyume cha sheria.

 

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Chanzo: mwananchi.co.tz