Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema: Maisha Yana Siri Kubwa

Z MBWA WA WEMA Wema Sepetu

Sun, 5 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SUPASTAA wa Bongo, Wema Isaac Sepetu au Tanzanian Sweetheart anasema kuwa, maisha yana siri kubwa hivyo yanahitaji uvumilivu mkubwa tofaui na hivyo unaweza kugombana na kila mtu kwenye ulimwengu huu.

Wema anasema kuwa, kuna mtu anaona wazi anamchokonoa na kumkera kupitia mitandao ya kijamii, lakini ukweli ni kwamba silaha kubwa ni uvumilivu na kunyamaza.

“Hakuna kitu kizuri kama kubeba uvumilivu kwenye moyo wako maana maisha yana siri kubwa mno na kufanya hivyo utaepusha mambo mengi na ndiyo maana watu siku hizi wanashangazwa na uvumilivu ambao niko nao kwa sasa na unazidi kunijenga,” anasema Wema ambaye kwa hivi sasa amepoa, tofauti na zamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live