Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wema: Ipo siku nitakuwa kiongozi wa Serikali

Wema Sepetu Res Wema: Ipo siku nitakuwa kiongozi wa Serikali.

Fri, 18 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji nguli wa filamu Bongo, Wema Sepetu amesema kuwa ndoto yake ya kuwa kiongozi wa Serikali bado anaishi nayo na atahakikisha anaitimiza hata kama ni baadaye sana.

Wema ambayer aliwahi kuwania kuteuliwa kugombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Ikungi, Singida mwaka 2015, amesema kuwa ataendelea kuwasaidia mabinti kupitia kampeni yake aliyoianzisha miaka hiyo ya Nasimama na Binti.

"Bado ndoto yangu ya kuwa kiongozi iko palepale, haikuishia 2015, bado natamani kuwa kiongozi wa Serikalini, iwe kuteuliwa au kugombea.

"Kampeni yangu ya (Nasimama na Binti) ni ishara nzuri kwangu, inanikutanisha na viongozi wengi wakubwa, huwezi jua pengine huu ndio ukawa mwanzo wangu huhudumu Serikalini," amesema Wema Sepetu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live