Supastaa wa Bongo Movies, Wema Sepetu wengi wanamfahamu kama mpenzi wa zamani wa Diamond Platnumz.
Baadhi ya wafuasi mitandaoni wamekuwa wakimkejeli Wema kwa kutokuwa na mtoto maishani mwake licha ya kuwa kwenye uhusiano na wanaume mastaa na wasi mastaa.
Baada ya kuchoshwa na komenti hasi za baadhi ya wafuasi wame, ameamua kuwatolea uvivu akiwaambia wanapaswa wamuache na maisha yake.
Kwa mujibu wa Wema, ujumbe wake uwaendee wale wote ambao wamekuwa wakimkosoa na kumkejeli.
“Yaani binadamu bwana, usipofanya wanasema, ukifanya pia wanasema....sasa sijui hata nifanye nn...Hebu mniache...” Anasema Wema.
Ni wazi kwamba, Wema alikuwa mpenzi wa Diamond; mapenzi yao yalitamaniwa na wengi, lakini hawakuweza kudumu.
Miezi michache iliyopita, Wema alikiri kwamba yupo singo, lakini anaweza kumpenda mtu.