Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Sanaa, Juliana Shonza amesema kifo cha msanii Mzee Majuto ni pigo kubwa kwa tasnia na serikali kwa ujumla.
Majuto alifariki dunia jana saa 2 usiku katika Hospitali y Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa tangu Julai 31.
“Hili limetupa funzo kuwa pamoja na jitihada ambazo binadamu yoyote anazifanya lakini uhai ni kudra ya Mwenyezi Mungu,” amesema.
Akizungumza leo Agosti 9 wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa Majuto, viwanja vya Karimjeee, Shonza ameema wasanii pamoja na serikali ilijitolea katika kuokoa maisha ya Mzee Majuto lakini haikuwezekana.
Pia ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa watu wanaoingia mkataba na wasanii kufuata taratibu.
Ameihakikishia familia yake kufuatilia haki zote za Mzee Majuto kwa kazi alizoingia mikataba na kampuni.
Soma Zaidi:
Magufuli,Kikwete, Polepole Mufti wawasili Karimjee kumuaga Mzee Majuto