Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mwijage ampa ushauri huu rapa Chemical baada ya kutazama ngoma yake mpya ‘Africa’s Heritage’

Video Archive
Thu, 31 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Charles Mwijage

Mwijage amefunguka hayo leo Mei 30,208 akiwa katika maonesho ya wiki ya maonesho ya utafiti yanayoendelea katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Chemical alitambulishwa kwa Waziri Mwijage chuoni hapo na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Kitivo Cha Urithi wa Utamaduni, Dkt. Eldidius Ichumbaki ambapo huwa wanamtumia kupitia kazi zake za kisanii kutangaza vivutio vinavyopatikana Tanzania.

Hukuona majina yote hadi ukaamua kujiita Chemical? kusema kweli mimi jina hilo kwangu halijakaa vizuri na hii kazi unayoifanya hapa Chuo Kikuu, nitakutafutia jina lingine si utaniruhusu?,” amemaliza Waziri Mwijage kwa kumuuliza swali Chemical hii ni baada ya kutazama video hiyo ya Africa’s Heritage.

Hata hivyo, Chemical amepokea ushauri huo wa kubadilisha jina kwa kusema kuwa atalipokea jina atakalopewa na Waziri Mwijage ila hawezi kufuta jina la Chemical kwani ndio Brand yake iliyomtangaza hadi kupata dili hilo chuoni hapo.

Tazama video za matukio mbalimbali kutoka Bongo5 hapa chini:



Loading...
Chanzo: bongo5.com