Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mwakyembe atua nyumbani kwa Wastara

1702 Mwakyembe1 TZW

Mon, 22 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe hapo jana( Jumapili) alikwenda kumtembelea msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma nyumbani kwake na kumjulia hali.



Mh.Waziri Mwakyembe ambaye aliambata na Katibu wa Bodi ya Filamu walifika nyumbani kwa muigizaji huyo kwa ajili ya kumjulia hali ambapo Waziri huyo aliahidi kumsaidia kiasi cha shilingi milioni. 1 kwa ajili kwenda India kwa ajili ya matibabu yake.

Hata hivyo Waziri Mwakyembe amewaomba wasanii wote nchini kuwa na moyo wa kujitolea na kumsaidia Wastara Juma ambae anahitaji kiasi cha shilingi milioni37, kwa ajili ya kurudi katika hospitali aliyokuwa akitibiwa hapo awali .

Kitendo cha Mh,Waziri kufika nyumbani kwa muigizaji huyo kimekuja baada ya msanii huyo kimekuja baada ya msanii huyo kuomba msaada kutokana na hali yake hiyo baada ya kupata ajali ya pikipiki miaka minne iliyopita na kumsababisha kukatwa mguu na ndipo alipowekewa mguu wa bandia ambao unahitaji kuhudhuria kliniki mara kwa mara lakini awamu hii alishindwa kurudi kutokana na kushindwa kupata fedha za kumrudisha hospitalini huko.

Chanzo: bongo5.com