Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Waziri Mkuu ampiga chini mkewe

Mgers Justin Trudeau Waziri Mkuu ampiga chini mkewe

Thu, 3 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau na mkewe Sophie wanatengana baada ya miaka 18, kufuatia "mazungumzo yenye tija na magumu".

Wanandoa hao walisema watasalia kuwa "familia ya karibu yenye upendo na heshima kubwa" katika mtandao wa Instagram. Walifunga ndoa huko Montreal mnamo 2005 na wana watoto watatu pamoja.

Katika taarifa, afisi ya Bw Trudeau ilisema kwamba ingawa wenzi hao walikuwa wametia saini makubaliano ya kutengana bado watajitokeza hadharani.

“Wamejitahidi kuhakikisha kuwa hatua zote za kisheria na kimaadili kuhusiana na uamuzi wao wa kutengana zimechukuliwa, na wataendelea kufanya hivyo kwa kusonga mbele,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza kuwa watakuwa likizoni kama familia wiki ijayo.

Wanandoa hao wameomba faragha kwa ajili ya "ustawi" wa watoto wao, Xavier, 15, Ella-Grace 14, na Hadrien, tisa.

"Tunasalia kuwa familia ya karibu yenye upendo mkubwa na heshima kwa kila mmoja na kwa kila kitu ambacho tumejenga na tutaendelea kujenga," Bw Trudeau, 51, na Sophie Grégoire Trudeau, 48, walisema.

Wameonekana pamoja hadharani mara chache sana katika miaka ya hivi karibuni, ingawa walihudhuria kutawazwa kwa Mfalme Charles III pamoja mwezi wa Mei na kumkaribisha Rais wa Marekani Joe Biden nchini Canada mwezi Machi.

Wakati Bw Trudeau alipochaguliwa kuwa waziri mkuu kwa mara ya kwanza mwaka wa 2015, wanandoa hao walionekana kwenye jarida maarufu la Vogue ambapo aliliambia wakati wa mwisho wa chakula cha jioni baada ya siku yao ya kwanza kukutana alisema, "Nina umri wa miaka 31, na nimekuwa nikikusubiri kwa miaka 31".

Katika ujumbe wa maadhimisho ya harusi kwenye Instagram mnamo Mei 2022, Bi Grégoire Trudeau aliandika kuhusu changamoto za mahusiano ya muda mrefu, akisema "tumepitia siku za jua, dhoruba kali, na kila kitu kilicho katikati".

Bw Trudeau pia amezungumza kuhusu changamoto katika ndoa yao, akiandika katika wasifu wake wa 2014: "Ndoa yetu si kamilifu, na tumekuwa na misukosuko migumu, hata hivyo Sophie anabaki kuwa rafiki yangu mkubwa, mshirika wangu, mpenzi wangu. Ni waaminifu kwa kila mmoja, hata kama inaumiza."

Wawili hao walianza kuchumbiana mnamo 2003, wakati Bi Grégoire Trudeau alipokuwa akifanya kazi kama mtangazaji wa TV.

Pia, anajulikana kwa kazi yake ya hisani kuhusu afya ya akili na matatizo ya ulaji. Trudeau ndiye waziri mkuu wa pili wa Canada kutangaza kujitenga akiwa madarakani.

Wa kwanza alikuwa baba yake, marehemu Pierre Elliott Trudeau, na mama Margaret Trudeau, ambao walitangaza kutengana kwao mnamo 1977 baada ya miaka sita pamoja. Baadaye waliachana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live