Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Mchengerwa ateua Kamati ya Mdundo wa Taifa wa Asili

Unnamed 1 3 Waziri Mchengerwa ateua Kamati ya Mdundo wa Taifa wa Asili

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amefanya uteuzi wa Kamati ya watu watakaoshughulikia suala la kutafuta Mdundo wa Taifa wa Asili.

Waziri Mchengerwa alifanya uteuzi wa kamati ya watu 11 ya kutafuta Mdundo wa Taifa wenye asili ya Kitanzania Kamati ambayo Mwenyekiti wake ni Dkt. Kedmon E. Mapana na Katibu wake Dkt. Herber Makoye.

Kamati zingine zilizoteuliwa ni Kamati ya Vazi la Taifa na Kamati ya Tamasha la 41 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo.

Aidha, Waziri Mchengerwa amezindua kampeni ya kuwatumia Wasanii na Wanamichezo inayojulikana kama #SensaBika ili wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye Sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti 23, 2022.

Waziri Mchengerwa amefanya ueuzi huo Julai 20, 2022 Uwanja wa Benjamin Mkapa katika hafla ya kuwaaga wachezaji wa Tanzania wanaokwenda kushiriki Mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Uingereza.

Amesema kutakuwa na tamasha kubwa la michezo, sanaa na utamaduni kwa ajili ya kuhamasisha Sensa ya watu na makazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live