Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wakamatwa kwa kufyatua risasi nyumbani kwa nyota wa Bollywood

Wawili Wakamatwa Kwa Kufyatua Risasi Nyumbani Kwa Nyota Wa Bollywood Wawili wakamatwa kwa kufyatua risasi nyumbani kwa nyota wa Bollywood

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Polisi nchini India wamewakamata wanachama wawili wa genge la wahalifu kwa shambulio la bunduki lililolenga nyumba ya mwigizaji wa Bollywood Salman Khan.

Nyota huyo ambaye ameshiriki katika filamu zaidi ya 100, alikasirisha genge la Bishnoi kwa kuwaua swara wawili zaidi ya miaka 20 iliyopita, polisi wanasema.

Genge hilo ni la madhehebu ya kidini ambayo humchukulia mnyama huyo kuwa mtakatifu.

Bw Khan hajadhurika, lakini hili ndilo tukio la hivi punde zaidi katika mfululizo wa vitisho ambavyo mwigizaji huyo amepokea katika miaka ya hivi karibuni.

Polisi mjini Mumbai walisema watu hao wawili walitumia pikipiki mapema Jumapili asubuhi na kufyatua risasi tano kwenye nyumba ya Khan katika kitongoji cha cha Bandra kabla ya kukimbia.

Vicky Gupta, 24, na Sagar Kumar Palak, 21, walikamatwa karibu na hekalu katika wilaya ya Kutch huko Gujarat Jumatatu usiku.

Kulingana na polisi, wawili hao walikiri kuhusika kwao katika tukio la ufyatuaji risasi nje ya Makazi ya Galaxy.

Chanzo: Bbc