Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Wauza kila kitu ili waishi wakisafiri kwenye meli

John Melody Henness.jpeg Wauza kila kitu ili waishi wakisafiri kwenye meli

Wed, 27 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanandoa waliojulikana kwa majina ya John Hennessee, mwenye umri wa miaka 76 na mkewe Melody Hennessee, mwenye umri wa miaka 64, wameamua kutumia muda wa maisha yao yote wakisafiri katika sehemu mbalimbali ulimwenguni kwa kutumia usafiri wa meli, ambapo walibainisha kuwa miaka mitatu iliyopita waliamua kuuza kila kitu walichokuwa nacho, ikiwemo biashara na makazi yao, kisha kununua gari maalumu lenye makazi ndani yake, ili waweze kusafiri wakizunguka sehemu mbalimbali za nchi ya Marekani.

Wanandoa hao wenye asili ya Florida nchini Marekani, wamesema baada ya kuzunguka kwa muda mrefu na gari walichoka kuendesha gari hilo ndipo walipoona tangazo kupitia mtandao wa facebook la safari ya siku 274, la kampuni ya meli ya Royal Caribbean, ndipo safari yao ya kudumu baharini ilipoanza.

Wawili hao ambao hadi sasa wametembelea sehemu mbalimbali ikiwemo Australia, New Zealand, Canada, Misri na Pasifiki ya Kusini, wamesema maisha ya ndani ya meli ni rahisi wakilinganisha na ya ardhini na kwamba hivi karibuni watachukua makazi ya kudumu kwenye meli ya kitalii ya Villa Vie ambayo 30% ya wasafiri wake watakuwa ni wakazi wa kudumu.

Wanandoa hao wamesema maisha hayo ni rahisi kwa sababu hayana gharama nyingi kama Bima ya gari, ankara za nyumba na bima za mali, na kwamba gharama za melini hajazijafikia hata nusu ya maisha ya ardhini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live