Tumezoea kuona wachongaji wa vinyago wakifanya ubunifu wa kuchonga sanamu zenye maumbile madogo kwa ajili ya kupamba sehemu mbalimbali.
Ifahamut ‘timu’ ya watu watatu Valerij Kunigel, DeividasTarulis na Virginijus Tarulis kutoka nchini Lithuania ambao waliweza kuvunja rekodi ya dunia mwaka huu mwezi Mei kwa kutengeneza sanamu ya nyoka yenye urefu wa mita 25.11, futi 82, nchi 4.
Timu hiyo iliunda sanamu hiyo ya mbao kwa takribani miaka 10 ambapo ndani ya miaka hiyo walikuwa wakiiboresha mpaka ilipokidhi viwango vya kuwa kwenye rekodi ya Dunia.
Kwa mujibu wa maelezo yao walieleza kuwa sanamu hiyo waliichonga kwa uangalifu na umakini wa hali ya juu kwa kutumia magongo makubwa huku vifaa vilivyopelekea sanamu hilo kuwa refu zaidi ni vipande vya mbao vilivyo unganishwa kwa kutumia gundi.