Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu wa Media tuache ku-support visivyokuwa vya msingi – Jabir Saleh, Mtangzaji E FM (+video)

Video Archive
Sat, 24 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Mtangazaji wa kipindi cha Ladha 3600 kutoka E FM, Jabir Saleh amesema moja ya vitu ambavyo vinarudisha muziki nyuma ni kiki za wasanii.



Jabir kuwa watu wa media ndio wanapelekea sana kuwepo kwa hilo ila endapo wataamua kusaidia wale wenye vipaji vya kweli.

“General kuhusu muziki wa Bongo kuna pande mbili, kuna watu wanapamba sana kuufikisha mbele na kuna vitu vinarudisha nyuma sana, mimi sio mpenzi wa kiki zinazofanyika kwenye muziki na kuaminisha watu kuwa wanafanya muziki, sasa hivyo hatuwezi kwenda mbele,” amesema.

“Kwa upande wa media, nafikiri sisi watu wa media kuna kazi moja ya kufanya, tuache ku-support visivyokuwa vya msingi na support vya msingi ukiona dogo ana kipaji basi msaidie,” amesisitiza.

Ameongeza kuwa kutokana na mambo hao miaka ya hivi karibuni wasanii wabongo wamezidiwa katika kupata tuzo na wale wa Nigeria baada kufanya vizuri hapo awali kitu ambacho hakileti picha nzuri.

Chanzo: bongo5.com