IKIWA leo ni siku ya pili tangu kuanza kwa tamasha la Sauti za Busara 2020 visiwani hapa watu wengi hujitokeza kuangalia burudani kutoka nchi mbalimbali za Bara la Afrika.
Idadi inaonekana kubwa kutokana na wageni hao kuujaza uwanja wa Mji Mongwe tofauti na siku ya ufunguzi wa tamasha hili, kwa wastani wa wageni hadi sasa wanakadariwa kufika 9000.
Leo kuna uwezekano mkubwa idadi ya wageni kuongezeka zaidi kutokana na wanamuziki wa Tanzania The Mafiki na Wakazi kutumbuiza kwani mara nyingi tamasha hili ikiwa siku ya wanamuziki Watanzania kupanda jukwaani huwa idadi ya wageni inaongezeka hasa kutoka Tanzania.
Kuna faida nyingi zinazopatikana kutokana na uwepo wa tamasha hili. Utalii wa makumbusho mbalimbali visiwani Unguja huingiza pato kubwa sanjari na wakazi wa Mji Mkongwe wa Zanzibar kunufaika na ujio wa wageni.
Burudani zinazotolewa na wanamuziki zinaonyesha kuwafurahisha watu waliohudhuria tamasha hilo kwani kila apandapo msanii jukwaani , watu hulipuka na shangwe za kelele wengine kupiga miruzi huku wengine kufuatilia nyimbo zinazoimbwa na wanamuziki hao.
Wasanii waliopanda leo jukwaani ni Apio Moro wa Uganda, Blinky Bill wa Kenya , Pigment, Swahili Encounters Zanzibar /Various
Pia Soma
- Lugha tatizo Sauti ya Busara
- Masanja anogesha Sauti ya Busara
- Sauti za Busara kumenoga, wasanii kila kona
Tamasha la Sauti za Busara ikiwa na kauli mbiu ya Paza Sauti, pinga unyanyasaji wa kijinsia limeanza Zanzibar Mji Mkongwe, Ngome Kongwe Februari 13 na litamalizika Februari 16 mwaka huu.