Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 100 wadai kufanyiwa unyanyasaji wa kingono na Diddy

Diddy Kuendelea Kusota Gerezani.png Watu 100 wadai kufanyiwa unyanyasaji wa kingono na Diddy

Wed, 2 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya watu 100 wanatarajiwa kumshtaki mwanamuziki wa rap Sean 'Diddy' Combs kwa unyanyasaji wa kingono, ubakaji na kutumiwa vibaya kingono, wakili wa Marekani amesema.

Wakili wa Texas Tony Buzbee amesema kuwa baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa waathirika ni pamoja na watoto wadogo ambao walinyanyaswa walipokuwa na umri wa miaka tisa.

"Hili ni jambo muhimu ambalo tunakusudia kulifuatilia kwa ukali," Bw Buzbee aliwaambia waandishi wa habari.

Wakili anayemwakilisha Bw Combs, Erica Wolff alisema rapa huyo "kwa msisitizo na kwa uwazi" anakanusha madai hayo, akisema ni "uongo na yenye lengo la kumharibia sifa".

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumanne, Bw Buzbee alisema yeye na timu yake "watafanya kila liwezekanalo kuwapata wahusika " katika madai ya unyanyasaji, au "mtu yeyote au taasisi yoyote ambayo ilishiriki au kufaidika na tabia hii ya kuchukiza".

Bi Wolff alisema katika taarifa kwa BBC kwamba Bw Combs "anatarajia kuthibitisha kuwa hana hatia na kujithibitisha mahakamani, ambapo ukweli utaelezwa kwa kuzingatia ushahidi, na sio uvumi".

Hatua hiyo ya kisheria ni ya hivi karibuni dhidi ya Bw Combs.

Bwana Combs alikamatwa wiki iliyopita na anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu ya ulanguzi wa ngono na biashara ya ngono. Kwa sasa yuko chini ya ulinzi wa shirikisho baada ya kunyimwa dhamana, ambayo anakata rufaa.

Hata hivyo Diddy amekanusha madai yote ya uhalifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live