Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wamkutanisha J. Lo na Ben Ben Affleck

Jlo X Ben Affleck Watoto wamkutanisha J. Lo na Ben Ben Affleck

Thu, 13 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuwepo kwa tetesi za mwanamuziki Jennifer Lopezi na mumewe Ben Affleck kutengana na kuuza nyumba yao waliyokuwa wakiishi, hatimaye wawili hao wamekutana tena katika mahafari ya mtoto wao.

Tovuti ya TMZ News imeeleza kuwa siku ya jana Jumatano Jennifer na Ben waliweka kando ratiba zao na kuhudhuria katika sherehe ya kuhitimu shule ya msingi ya mtoto wao aitwaye Samwel.

Wanandoa ambao mpaka sasa ndoa yao inaukakasi licha ya kujumuika katika sherehe hiyo bado walikuwa na mipaka kati yao hali ambayo imezidi kuwapa maswali watu baada ya kukataa kupiga picha ya pamoja.

Hata hivyo mwimbaji huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 54 na mumewe mwenye umri wa miaka 51, pamoja na kuonekana penzi lao limekwisha lakini huenda bado kuna mapenzi kati yao hii ni baada ya kuonekana wakiwa wamevalia pete za ndoa.

Ikumbukwe kuwa wawili hao walianza mahusiano mwaka 2002 na kutengana kwa mara ya kwanza mwaka 2004, lakini Julai mwaka 2021 walithibisha kurudiana hivyo mwaka 2022 waliweza kufunga ndoa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live