Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto saba wamkimbiza mchakamchaka Patcho Mwamba

46959 Pic+patcho

Mon, 18 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Msanii wa muziki wa dansi, Patcho Mwamba amesema idadi ya watoto saba alionao inamfanya kukimbizana ili kuwatengenezea maisha mazuri ya hapo baadaye.

Patcho ambaye pia ni muigizaji wa filamu alilimbia Mwananchi kwamba, kila mzazi anapokuwa na mtoto anatamani kuona ndoto zake zinakamilika na kuhakikisha anatumia kila fursa inayoonekana mbele yake ili kufanikisha hilo.

Hilo limechochea kuhakikisha anatumia muda wake vilivyo katika kufanya kazi za kuimba na wakati huohuo filamu bila kuathiri nyingine.

Patcho ambaye amecheza filamu mbalimbali ikwemo Bado Natafuta, Young Billionaire, This is It’, Ndoa ya Utata na nyingine nyingi, alisema ndio maana anatumia saa chache kulala na kutoa mfano kuwa hutoka kwenye shoo saa kumi usiku na wakati huohuo asubuhi anahitajika kwenda location kwa ajili ya kupiga picha za filamu.

“Ukiangalia ni kazi ngumu kidogo kwani kama binadamu natakiwa nipate muda wa kupumzika, lakini nikipumzika kuna watoto hawa saba wananiangalia mimi, sina cha kufanya isipokuwa ni kujitosa ili kuwatengenezea kesho yao,” alisema Patcho ambaye ni mwanamuziki wa bendi ya FM Academia.

Wito wake kwa wasanii wenzake ni kuheshimu kazi ya sanaa kama ilivyo kazi zingine.

Alieleza kuwa kuna baadhi wanapopata kazi hata kufika kwa wakati kambini kwao ni kazi.

Tabia kama hizi alieleza kuwa zitakuja kuwagharimu hapo baadaye watakapokutana na watu wengine wanaopenda jambo lao lifanyike kwa muda uliopangwa, ambao hawajali ukubwa wa jina alilo nao msanii katika tasnia kitu ambacho wasanii wengi wa Bongo wanaringia.

Mbali ya kuwa mwimbaji na muigizaji, Patcho pia ni mbunifu wa mavazi na mwandishi wa nyimbo na miswada ya filamu.



Chanzo: mwananchi.co.tz