Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Wateja walioagiza gari hii..! kusubiri kwa miezi 6

SU 7 Max SU7 Max

Tue, 2 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku chache tu baada ya kampuni ya China ya kutengeneza simu Xiaomi kuzindua gari lake la kwanza linalotumia umeme (EV), wanunuzi wameambiwa watalazimika kusubiri hadi miezi sita kupata gari waliloagiza.

Taarifa zilizojitokeza kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha kampuni hiyo ikiwaambia wateja wake kuwa huenda wakalazimika kusubiri hadi wiki 27 kupata gari la SU7 Max.

Kampuni hiyo awali ilisema ilipata wateja 88,898 ndani ya kipindi cha saa 24 ilipotangaza kupokea manunuzi siku ya Alhamisi.

Xiaomi haikuwa tayari kusema lolote kuhusu taarifa hizi ilipoulizwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza.

Kampuni hiyo kubwa ya teknolojia, ambayo ni ya tatu duniani kwa uuzaji wa simu janja, ikiwa na takriban hisa asilimia 12 kwenye soko ulimwenguni, inapambana sasa na washindani wengine wa EV kama vile Tesla na BYD katika soko kubwa la magari ya aina hiyo.

Gari la kawaida aina ya SU7 linauzwa kwa yuan 215,900 sawa na dola 29,872 (Shs 76,621,680) na lile aina ya Max ni yuan 299,900 (TShs 1,063,842,99).

Nchini China, Tesla Model 3 inauzwa kwa yuan 245,900 (TShs 87,228,740).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live