Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watano wajitokeza kubadili shepu Muhimbili

ShapeWA0007 Watano wajitokeza kubadili shepu Muhimbili

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof Mohammed Janabi amesema watu watano wamejitokeza kujisajili, ili kupata huduma ya kurekebisha maumbo huku akisema jambo hilo linalenga matibabu.

Hata hivyo Prof Janabi amesema hadi sasa ni mtu mmoja tu, ambaye ameomba kufanyiwa huduma hiyo kwa ajili ya urembo, wakati wengine ni kwa ajili ya matibabu, ambapo awamu hii watafanya kwa watu sita hadi 10

"Tunategemea wahitaji zaidi kwa mara ya kwanza hatuwezi kufanya wengi na muda ni mdogo tutaona kwasababu tutafanya nyingine na wenzetu wa Afrika Kusini mwishoni mwa mwaka,"ameieleza Prof Janabi.

Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Muhimbili-Mloganzila Dk Erick Muhumba ameiambia HabariLEO kuwa wanafanya upasuaji wa aina mbili ambao wa kwanza ni upasuaji wa kupunguza uzito na upasuaji rekebishi.

Ameainisha kuwa gharama za upasuji zinatofautiana kuanzia Sh 150,501,171 hadi Sh 225,699,173, ambapo inategemea na mtu na aina ya upasuaji na kadiri wanavyotofautiana na gharama zinatofautiana hata kama upasuaji ni mmoja. "Hayo ni matibabu kwa sababu kuna mtu wana kisukari shida yake ni unene anapofanya upasuaji inamsaidia ,lakini pia kupunguza unene inalinda, kuna magonjwa ya moyo, presha, figo na mengine yanalinda, kiasi kubwa ni matibabu,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live