Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Watakiwa kupaza sauti kupambana na ndoa za utotoni

82304da228405663ef0cf4c30c6853fb.png Watakiwa kupaza sauti kupambana na ndoa za utotoni

Thu, 18 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WABUNGE wanawake wametakiwa kupaza sauti ya kupambana na ndoa za utotoni ili kusaidia watoto hao kutimiza malengo yako.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa taasisi ya Msichana Initiative wakati akitoa mada kwenye mkutano wa majadiliano na Mtandao wa Wanawake, Katiba, Uchaguzi na Uongozi chini ya Uratibu wa Mfuko wa Udhamini wa Wanawake Tanzania ( WFT) na Wabunge wanawake mjini hapa.

Alisema tatizo la mimba za utotoni ni kubwa na kuwa ili kulimaliza ni vyema pia ukawepo ushirikiano na wabunge wanawake.

Alisema takwimu zinaonesha kuwa kati ya wasichana wa tano, wawili wanaolewa wakiwa bado hawajafikisha umri wa miaka 18.

Naye Naibu Spika, Dk Tulia Ackson aliutaka mtandao huo kuwapatia takwimu za matukio ya ukatili wa kijinsia ili wajue ni jinsi gani wanapaza sauti zao.

" Kupitia takwimu hizo tutaweza kutambua ni wapi tumekwama, tufanye nini, tupige kelele namna gani. Tumeambia kati ya wasichana wa tano, wawili wanaolewa wakiwa bado hawajafikisha umri wa miaka 18, lakini hatujaambiwa hao watano wapo shule au la maana tunajua kuna waliopo shuleni na wengine hawasomi. Tukipata takwimu za kutosha zilizoeleza kila kitu tutakuwa na nguvu ya kujenga hoja kule bungeni."

Naye mjumbe wa mtandao huo, Agness Lukanga alisema lengo la kukutana na wabunge ni kubadilishana mawazo juu ya kulinda haki za msichana na mwanamke.

" Popote mtakapokuwapo (wabunge) na mtakachokiona kinachohusu mwanamke tambueni kuwa ni wajubu wenu kushughulikia. Chochote kitakachofanywa bungeni mkiangalie kwa mtazamo wa kijinsia, kama vile bajeti zinazotengwa na zinawanufaisha vipi wanawake pamoja na kuzingatia masuala ya 50 kwa 50 kila hatua."

Akichangia, Mbunge wa Viti Maalumu, Salome Makamba (CHADEMA) alihoji kinachofanywa na mtandao huo kuhusu unyanyasaji wa kijinsia wakati wa kampeni za uchaguzi.

Naye mbunge wa jimbo la Tanga Mjini, Ummy Mwalimu(CCM) aliungana na Makamba kuhusu unyanyasaji wa kijinsia uliojitokeza kipindi cha kampeni.

Mwalimu ambaye ni Waziri wa Muuungano na Mazingira alisema kuna haja ya kuongeza nguvu kupambana na unyanyasaji, udhalilishaji wa kijinsia unaofanyika katika maeneo mbalimbali.

"Kama alivyosema mh Salome, wakati naenda kugombea Tanga Mjini kuna watu walisema msimchague kwa sababu ni mwanamke, lakini nilipata nguvu kubwa ya wananwake ambao ndio walisema tunaenda kumsimamisha mgombea mwanamke na kweli likatimia," alisema.

Alisema licha ya kuwa nguvu kubwa aliipata kutoka kwa wanawake lakini kwenye kampeni hakuwaacha wanaume hivyo katika upambanaji wa ukatili wa kijinsia wanaume wasiachwe nyuma.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Ritha Kabati (CCM) alisema ili kukabiliana na ukatili wa kijinsia unaojitokeza kwa wanafunzi, Serikali na wadau wanatakiwa kuanzisha madawati ya kijinsia shuleni.

Chanzo: habarileo.co.tz