Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watakaoshiriki tamasha la pasaka waanza kutajwa, yupo Tumaini Akilimali wa Kenya

Msama Pasaka Watakaoshiriki tamasha la pasaka waanza kutajwa, yupo Tumaini Akilimali wa Kenya

Sat, 25 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Maandalizi ya tamasha la Pasaka yamepamba moto na waimbaji watakaoshiriki wameanza kutajwa wakiwemo wa ndani na nje ya nchi.

Majina ya waimbaji hao yameanikwa leo Ijumaa Februari 24, 2024 na Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion ambayo ndio waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama alìpozungumza na waandishi wa habari.

Amewataja waimbaji hao ambao tayari wamethibitisha ushiriki wao kuwa ni pamoja na Tumaini Akilimali wa Kenya, Joshua Ngoma wa Rwanda na Masi Masilia wa nchini Congo ambaye huyu ni mara yake ya kwanza kutua Tanzania.

Kwa upande wa waimbaji wa Tanzania yupo Upendo Nkone, Ambwene Masongwe, Joshua Mlelwa na Zabron Singers.

Akielezea kuhusu maandalizi tamasha hilo, Msama amesema yanaendelea na kuahidi kuwa litakuwa tamasha la kimataifa na kubainisha kuwa wamekuja kivingine baada ya kutofanyika kwake kwa miaka saba.

"Leo tunatambulisha wasanii watakaoshiriki tamasha hilo litakalofanyika Aprili 9 mwaka huu katika uwanja wa uhuru Dar es Salaam.

"Niwaambie tu tamasha litakuwa na waimbaji wengi wa kimataifa ambao hawajawahi kukanyaga hapa Tanzania na waimbaji manguli wa hapa nchini hivyo sio la kukosa," amesma Mkurugenzi huyo .

Hata hivyo amesema bado wapo kwenye mazungumzo na waimbaji wengine kutoka nchini Afrika Kusini, Uingereza na Marekani.

"Tunaposema tumerudi tena tunaamaanisha, jiandaeni na tamasha zuri, tamasha la kihistoria,"

Katika taasha hilo Msama amesema pia watazungumzia miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani ambaye kila wakati amewataka Watanzania kumuombea lakini pia watalitumia kuiombea nchi kuepukana na majanga ya asili ikiwemo kimbunga matetemeko ya ardhi na mafuriko.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati maandalizi ya tamasha hilo, Emmanuel Mwabisa amesema waimbaji siku hiyo wataimba live na tayari wameshaanza kutuma 'technical reader' zao na kueleza kuwa wanashukuru wamepata kampuni yenye utaalam wa kufunga vyombo vya live

Chanzo: Mwanaspoti