Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wastara alilia mguu wake

94dee238e6ebf5afcc6271328a0ef515 Wastara alilia mguu wake

Thu, 18 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MWIGIZAJI wa filamu, Wastara Juma ameeleza kwa uchungu namna familia yake ilivyomficha walipozika mguu wake aliokatwa mwaka 2009 baada ya kupata ajali ya pikipiki.

Mwaka huo Wastara akiwa na mchumba wake marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ walipata ajali ya pikipiki maeneo ya Tabata, Dar es Salaam iliyosababisha kuumia vibaya mguu wake wa kushoto na kukatwa.

Katika mahojiano maalum jana, msanii huyo alisema tangu kipindi hicho aliomba familia yake kumweleza wapi walipopeleka mguu wake lakini hadi leo bado hawajamwonesha.

“Mpaka leo familia yangu haijakubali kunieleza walizika wapi mguu wala mume wangu wakati huo hakujua ulipelekwa wapi,” alisema kwa uchungu huku akifuta machozi.

Msanii huyo pamoja ulemavu alionao amekuwa akitembelea mguu bandia na kuendelea na shughuli zake za sanaa na za kijamii.

Licha ya kupata ajali hiyo, marehemu Sajuki hakumuacha msanii huyo alimuoa na kuishi naye hadi mauti yalipomkuta.

Chanzo: habarileo.co.tz