Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wastara akerwa na mama Kanumba

140f9d66920ad857e2bea60283edc56a Wastara akerwa na mama Kanumba

Mon, 8 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MWIGIZAJI wa filamu ambaye hivi karibuni alizindua taasisi yake ya kusaidia watoto ya Wastara Foundation, Wastara Juma amesema amechoshwa na tabia ya mama Kanumba kuendelea kuwalalamikia watu juu ya kifo cha mwigizaji huyo kwa takribani miaka 9 mfululizo.

Wastara alisema tangu muigizaji huyo afariki dunia mwaka 2012, mama huyo amekuwa akilalamikia watu kusababisha kifo chake hasa shutuma zote akimtumia mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Alisema hataki kuamini kama mwigizaji huyo hakuwahi kumuomba msamaha mama huyo, ingawa hajui ni msamaha wa aina gani ambao mama huyo anauhitaji kutoka kwa Lulu.

“Kikubwa unachotakiwa kufanya ni kusamehe na kusahau kuhusu Lulu na usiwe unamtia mdomoni kila wakati unaojiskia wewe sio sawa watu hawakutafsiri vizuri wanakusema vibaya na unaonekana una roho mbaya” alisema

Chanzo: habarileo.co.tz