Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasiolipa mirabaha wapelekeni Mahakamani-MwanaFA

Wasiolipa Mirabaha Wapelekeni Mahakamani MwanaFA Wasiolipa mirabaha wapelekeni Mahakamani-MwanaFA

Fri, 17 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma maarufu MwanaFA ameagiza makampuni na maeneo yanayotumia kazi za sanaa na ubunifu kujinufaisha kibiashara kuhakikisha kuwa yanalipa mirabaha na madeni ya nyuma yanayodaiwa huku akiiagiza Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) iwachukulie hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha Mahakamani wote waliokaidi kulipa.

Hamis Mwinjuma ametoa maagizo hayo alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kwa ajili ya kujionea shughuli zinazofanywa na ofisi hiyo.

Hatua hiyo inakuja baada ya COSOTA kuwasilisha taarifa inayoonesha kuwa baadhi ya makampuni nchini yamekuwa yakikaidi kwa makusudi kulipia mirabaha huku yakiendelea kutumia kazi za sanaa katika biashara zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live