Posho za watu wasiokuwa na ajira zitaongezwa hadi (Euro 609) takribani TSh. Milioni 1.6 kwa mwezi kuanzia mwaka ujao nchini Ujerumani kulinganisha na malipo ya sasa ya (Euro 502)
Waziri wa ajira Hubertus Heil amesema watu zaidi ya milioni tano watanufaika na ongezeko hilo la asilimia 12.
Waziri huyo ameeleza kuwa watu hapa nchini Ujerumani wanaweza kuitegemea serikali inayojali ustawi wa jamii na hasa katika nyakati za shida na misukosuko.
Serikali ya mseto ya Ujerumani ilipitisha mageuzi makubwa katika mfumo wa ustawi wa jamii mwaka uliopita kwa manufaa ya watu ambao wamekaa muda mrefu bila ya ajira. Posho kwa ajili ya watu wenye watoto pia zinatarajiwa kuongezwa