Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Wasichana watatu kati ya 10 wanaathirika na ndoa za utotoni

Wasichanaapiic Data Wasichana watatu kati ya 10 wanaathirika na ndoa za utotoni

Sat, 17 Sep 2022 Chanzo: Mwananchi

Imeelezwa wasichana watatu kati ya 10 wenye umri chini ya miaka 18 wanaingia kwenye changamoto ya ndoa za utotoni nchini.

Hayo yamesemwa leo Jumamosi Septemba 17, 2022 na Mkurugenzi Mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Zlatan Mullisic katika maadhimisho ya kampeni ya  Binti inayowahusisha wadau wote wanaoshughulika na masuala ya kupinga ndoa za utotoni.

Zlatan ametaja athari anazokumbana nazo msichana anayeolewa katika umri mdogo kiafya, kiuchumi, kijamii, kisaikolojia na kuondolewa utu wao.

“Wasichana watatu kati ya 10 wanaolewa chini ya umri, hii inamfanya msichana apoteze fursa za elimu na ujuzi wa kazi, kupata ya maambukizo ya virusi vya ukimwi (vvu) au magonjwa ya zinaa, kunyanyasika kisaikolojia, kimwili, kijinsia na hivyo kudumishwa kwa haki na utu wao.

“Hili lazima tulikemee kwakuwa linaathiri kuyumba kiuchumi na kudumu katika umasikini, vifo vya watoto wachanga na watoto wa kike pindi wanapojifungua kwa kuwa viungo

vyao vya uzazi bado havijakomaa pia inaongeza  vifo vya wajawazito na kuharibika kwa mimba,” amesema Zlatan.

Mhariri wa Habari wa gazeti la Mwananchi na mwakilishi wa Jukwaa la wahariri, Lilian Timbuka amesema vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kutoa elimu ili kusaidia kutokomeza ndoa za utotoni.

Amesema kwa kuwa wanaoathirika zaidi ni wasichana wanaoishi pembezoni hivyo juhudi kubwa za wamiliki na waandishi wa habari nikupaza sauti kuwasemea wale ambao hawawezi kujisemea ambayo ni kazi ya kalamu zao.

“Sauti isiyo na sauti inapazwa na vyombo vya habari, lakini tunahamasisha kampeni hizi ziende zaidi vijijini huko ndiko athari hizi zinatokea zaidi na wazazi, walezi na wasichana wenyewe hawana taarifa,” amesema Timbuka.

Mwakilishi wa viongozi wa dini na Mkuu wa jimbo la Magharibi-Dayosisi ya mashariki na pwani KKKT, Anta Muro amesema viongozi wa vyombo vya dini wanaunga mkono kampeni hiyo kwa lengo la kupambana na tatizo la watoto kuolewa katika umri mdogo.

Wadau mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo ya BintiDay walitoa maoni yao wakisema sheria ifanyiwe mabadiliko na umri sahihi wa kuolewa unapaswa kuwa miaka 21.

Wiki ijayo Kamati za Bunge za Maendeleo ya Jamii pamoja na Kamati ya Sheria na Katiba zitaketi pamoja kwa ajili ya kufanya marekebisho ya Sheria ya Ndoa.

Chanzo: Mwananchi