Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washukiwa wa mauaji ya rapa wa Afrika Kusini AKA wafikishwa mahakamani

Washukiwa Wa Mauaji Ya Rapa Wa Afrika Kusini AKA Wafikishwa Mahakamani Washukiwa wa mauaji ya rapa wa Afrika Kusini AKA wafikishwa mahakamani

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Watu watano kati ya wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya rapa wa Afrika Kusini, Kiernan Forbes, maarufu AKA, na rafiki yake wa karibu, mpishi maarufu na mjasiriamali Tebello "Tibz" Motshoane, wamefikishwa mahakamani.

Kesi hiyo, ambayo ilirushwa moja kwa moja kwenye vituo kadhaa vya TV vya Afrika Kusini, sasa imeahirishwa hadi wiki ijayo.

Watano hao waliingia kizimbani kwa mara ya kwanza, kusimama wakitazama chini wakiwa wamefunika nyuso zao.

Mwendesha mashtaka aliwasomea mashitaka 10 yakiwamo ya mauaji, kula njama ya mauaji, kujaribu kuua na kumiliki silaha kinyume cha sheria.

AKA na Motshoane walipigwa risasi nje ya mkahawa mmoja katika mji wa pwani wa Durban mwaka mmoja uliopita.

Mauaji hayo yaliishangaza Afrika Kusini, ambayo ina viwango vya juu zaidi vya uhalifu duniani.

Kesi za mahakama zilitazamwa na babake AKA, Tony Forbes, Waziri wa Polisi Bheki Cele na kamishna wa polisi wa jimbo hilo Lt Jenerali Nhlanhla Mkhwanazi.

Jimbo liliomba kuahirishwa kwa uchunguzi zaidi.

Ilisema inapanga kuongeza washukiwa wengine wawili waliokamatwa hivi karibuni huko Eswatini kuhusiana na kesi hiyo.

Chanzo: Bbc