Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Washtakiwa kwa kuiba, kula ndege aina ya Swan

Mute Swans Heart Washtakiwa kwa kuiba, kula ndege aina ya Swan

Thu, 1 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vijana watatu wa jimbo la New York walimuua swan ambaye hufanana sana na bata wa kawaida na bata bukini, nakumpika kwaajili ya chakula cha jioni na kuwakamata watoto wake wanne baada ya kudhani kuwa ni bata kwenye kidimbwi cha maji kilichohifadhiwa, polisi walisema.

Faye swan inadaiwa aligeuzwa kuwa chakula cha jioni na vijana katika Siku ya Kumbukumbu huko Manlius kijiji cha watu 4,600 katika vitongoji vya Syracuse, ambapo ni kwenye makaazi na kwenye bwawa ambalo hufuga swans wanaomilikiwa na mji na inasemekana wameishi tangu 1905.

Polisi walisema Jumatano kwamba vijana hao marafiki watatu, wenye umri wa miaka 16, 17 na 18.

“Hawakujua kwamba alikuwa swan, na hawakujua kwamba hakuwa mnyama wa porini, kwamba alikuwa akimilikiwa na Kijiji cha Manlius,” Manlius Police Sgt. Ken Hatter alisema.

Washukiwa wote watatu ikiwa ni pamoja na mkubwa, ambaye alitambuliwa kama Eman Hussan wa Syracuse walishtakiwa kwa uhalifu mkubwa wa ulahgai na uongo, kula njama na makosa mengine ya jinai, iliripoti CNY Central.

Swans ni ndege wa familia Anatidae ndani ya jenasi Cygnus na familia wa karibu wa swans ni pamoja na bata bukini au hufanana sana na bata wa nyumbani na ni miongoni mwa ndege wakubwa zaidi wanaoruka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live