Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washereheshaji waaswa bei elekezi

MCCCC Washereheshaji waaswa bei elekezi

Fri, 19 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWENYEKITI wa washereheshaji Mkoa wa Mbeya, Charles Mwakipesile, amewahimiza kuzingatia bei elekezi waliyokubaliana ili kuendelea kutunza heshima ya kazi yao.

Mwakipesile alitoa kauli hiyo juzi, kuwa siku kadhaa zimepita tangu Rais John Magufuli avunje Bunge mjini Dodoma, na kuagiza shule zote nchini zifunguliwe pamoja na shughuli zote ziendelee zikiwamo harusi na sherehe nyingine.

Kutokana na kauli hiyo, aliwatahadhari wenzake kuzingatia makubaliano yako kwamba mshereheshaji yeyote anatakiwa kufuata bei elekezi ambayo kima cha chini shilingi milioni moja kwa ukumbi wa kawaida na mkubwa ni Sh. milioni 1.5 na sio kukubali kulipwa kiasi kidogo ambacho kinashusha hadhi ya kazi hiyo.

“Tunampongeza Rais wetu kwa kuruhusu sherehe ziendelee kama kawaida, nawakumbusha ma-MC wenzangu tujitunzie heshima tuheshimu makubaliano yetu tuache njaa hata kama shughuli zilisitishwa, tulikubaliana yeyote atakayekiuka atakuwa amejiondoa kwenye umoja wetu,” alisema Mwakipesile.

Pia aliwaomba wamiliki wa kumbi za hoteli kuwa na orodha ya washereheshaji wote ikiwa ni njia moja wapo ya kujitangaza kibiashara.

Aliongeza wateja wao wanapaswa kufahamu kuwa bei ya kuanzia shilingi milioni moja ni ndogo kwani wanalipa ushuru na nyingine inakatwa kwenye Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Aidha, alipiga marufuku uvaaji holela wa mavazi ambayo yanashusha hadhi ya mshereheshaji kwa maelezo kuwa baadhi wamekuwa wakitia aibu kutokana na uvaaji wao ambao hauendi na wakati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live