Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasanii wasiopenda kutangaza vivutio vya utalii Tanzania wakosolewa

74734 Utalii+pic

Mon, 9 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji mstaafu Thomas Mihayo amewatolea uvivu wasanii na watu maarufu wasio tayari kutangaza vivutio vya utalii hadi wawezeshwe na Serikali kuvifikia vivutio hivyo.

Amesema mwenendo huo unaashiria kuwa wasanii hawajiamini na wanashindwa kutumia ukubwa wa majina yao kuonyesha uzalendo.

Jaji Mihayo ameyasema hayo jana Jumamosi Septemba 7, 2019 wakati wa hafla ya chakula cha usiku iliyowakutanisha wasanii, wadau wa utalii na watendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii ili kujadili kwa pamoja namna ya watu maarufu wanavyoweza kutumika kutangaza vivutio vya utalii.

“Nakerwa na watu wanaoomba kuwezeshwa kwenda kwenye vivutio vya utalii, hivi ukifanya tamasha ukaweka kiingilio Sh5000 hupati fedha za kwenda huko? Hili ni suala la uzalendo lakini nashindwa kuelewa kwa nini hamjiamini kuwa mnaweza kufanya kitu kikubwa kupitia majina yenu.”

“Nasisitiza uzalendo, Watanzania wenyewe tuwe na hamu ya kuifahamu nchi yetu na kuwa mabalozi wa kuwaambia watu wengine kuhusu vitu vizuri vinavyopatikana hapa.”

Akizungumza kwa niaba ya waalikwa msanii Mwijaku aliwataka wasanii wenzake kujitoa na kuwa mabalozi wa kutangaza kazi zinazofanywa na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo bila kutegemea kulipwa.

Pia Soma

Advertisement

Katika hafla hiyo,  Mwijaku alitangaza kujitolea kuwa balozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) akiahidi kutumia ukurasa wake wa Instagram kutangaza kuhusu misitu 17 iliyopo chini ya taasisi hiyo na vivutio vilivyomo ili kuwahamasisha watu kutembelea.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz