Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasanii, wadau waungana kuokoa maisha ya Haitham Kim

Haitham Kim Wasanii, wadau waungana kuokoa maisha ya Haitham Kim

Fri, 1 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa sasa Hali ya afya ya msanii wa Bongo Fleva, @haithamkim ni mbaya, yupo chini ya uangalizi, Chumba Cha wagonjwa mahututi (ICU) na anahitaji msaada tayari wasanii mbalimbali wametumia mitandao yao ya Jamii kuomba wadau na mashabiki watume michango yao.

Baadhi ya wasanii hao ni pamoja na Alikiba, Billnass, Aunty Ezekiel na Harmonize ambaye pia amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan amsaidie.

Ifahamike kuwa Mume wa Haitham, Bryson Peter Mtei maarufu @niiteboshen alitoa taarifa hii

"Napenda kuwajulisha kwamba mke wangu @haithamkim yuko katika hali mbaya sana ya ugonjwa. Afya yake imezorota na tunahangaika sana. Tunawaomba kwa pamoja tumuombee, maombi yenu niuhimu sana kipindi hiki, na msaada wenu wakati huu mgumu.

Ugonjwa wake umetuletea changamoto kubwa kihisia na kifedha kwa familia yetu. Tunafanya kila tuwezalo kumuhudumia vyema, lakini gharama za matibabu ni kubwa sana. Iwapo kuna mtu yeyote anayeweza kutoa msaada wowote, iwe ni kifedha au vinginevyo, itakuwa ni jambo lenye shukrani kubwa. (0746747726 BRYSON PETER MTEI)". Hivyo mdau karibu kuchangia

Kutangaza Biashara Yako na Msasa Online WhatsApp Namba bofya hapa 0758 379 300

Chanzo: www.tanzaniaweb.live