Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasanii wa zamani wajitambue, muziki umebadilika – Alikiba

4440 16906856 1822214474721420 6467752781024329728 N TZW

Mon, 12 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki Bongo, Alikiba amesema licha ya wasanii wa zamani kupitia changamoto nyingi katika muziki huo wanapaswa kuelewa kwa sasa muziki umebadilika.



Hitmaker huyo wa ngoma ‘Seduce Me’ ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa wasanii wa zamani wameutoa muziki mbali ila wanapobadilika wanakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kunufaika nao kwani muziki wa sasa una fedha ukilinganisha na zamani.

“Napenda changamoto ambazo wanakutana nazo wasanii wa zamani, sasa hivi wajitambue kuwa muziki umebadilika sana. Ukiangalia wao wameutoa muziki mbali kitu ambacho tunashukuru, sisi tumeukuta tu tunauendeleza,” amesema.

“Sisi tunaona wanatupatia tu faidi kuliko wa zamani, zamani muziki ulikuwa hauna hela ila sasa hivi una hela japokuwa mimi mwenyewe nimeutoa huko huko,” ameongeza.

Alikiba hajatoa ngoma yoyote kwa mwaka huu, ngoma ya mwisho kutoa ni Seduce Me ambayo ilitoka August 25, 2017, na ngoma ya mwisho kushirikishwa ni Single ya Abdu Kiba.

Chanzo: bongo5.com