Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasanii wa kuangaliwa 2021

WhatsApp Image 2021 05 25 At 11.36.53.jpeg Wasanii wa kuangaliwa 2021

Tue, 25 May 2021 Chanzo: eatv.tv

Kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva kila mwaka kimeendelea kupiga hatua kwa kuzalisha nyota wapya ambao wamekuwa na mchango mkubwa sana kwenye maendeleo ya burudani nchini.

Baadhi yao wamefanikiwa kuachia kazi kadhaa na kutawala kwenye chart mbalimbali za muziki huku idadi ya wasanii wa kike wapya ikionekana kuwa kubwa ukilinganisha na miaka kadhaa ya nyuma.

Wafuatao ni baadhi ya nyota hao;



Angella – Akiwa tayari ameanza kuonja ladha ya mafanikio ya muziki hapa nchini, muziki wa Angella sasa unavuka mipaka kwa kuchezwa kwenye vituo vya Redio na Tv, huku siku za hivi karibuni msanii huyu wa Konde Music Worldwide alionekana akiwa studio akirekodi nyimbo na msanii mkongwe Awilo Longomba na Victoria Kimani ikiwa ni ishara tosha ya kuonesha ni  msanii mwenye malengo.



Saraphina – Ni mwanamke mwenye uwezo mkubwa na sauti mahiri, aliwahishiriki mashindano ya kutafuta vipaji ili kupata tundu la kutobolea kimuziki.

Mwaka huu Saraphina amefanikiwa kuachia nyimbo mbili ‘In Love na Sitaki Tena’ ambazo zimeleta ladha mpya sokoni.



Phetty –  Inawezekana masomo yake ya udaktari wa Binadamu ndio yalifanya dunia ichelewe kumfahamu, Phetty alipata umaarufu kwa wimbo wake ‘Asali’ ambao una mwaka mmoja tangu utoke.

Anasifika kwa sauti nzuri inayotoka moyoni na kujielezea kwa ustadi mkubwa katika mtindo wa kipekee na muziki wake umepokelewa vema na wafuasi wake.



Mattan – Yeye hujiita SUMU, ni ingizo jipya kwenye muziki wa RnB bongo, sauti ya kijana wa mjini na uandishi wake hakika unahamasisha kumpa nafasi kubwa sana ya kumzingatia, hakika hakuna kitakacho msimamisha kama atakuwa na mwendelezo mzuri.



Lil Dwin – Rapper wa kizazi kipya ambaye amesikika kwenye projects kama ‘Day One ya Salmin Swaggz, Instructions ya Paul Maker’ na kwa sasa ni msanii wa Bongo Records akipikwa kwenye chungu kimoja walichopikiwa wakongwe kama Jay Moe, The late Mangwair na wengine kibao.



Mapanch Bmb – Amefanya unyama mkubwa sana kwenye wimbo wake ‘Yekwe’ kwa aina yake ya uimbaji, Wanene Studios walikiona kipaji chake na kisha kum-sign, kama akipewa nafasi bila shaka Taifa litajivunia hapo baadae.
Chanzo: eatv.tv