Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasanii wa injili kukiwasha Arusha

Msama Promo Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Alex Msama

Sat, 12 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Tamasha la kuiombea nchi na kumwombea Rais Samia Suluhu Hassan linatarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu Jijini Arusha ambapo wasanii mbalimbali wa muziki wa injili wanatarajia kutumbuiza.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Ijumaa Novemba 11, 2022 jijini Arusha Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Alex Msama amesema maandalizi kwa ajili ya tamasha hilo yanaendelea vizuri.

Amesema lengo la tamasha hilo ni kuiombea Nchi pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan Mwenyezi Mungu ampe afya njema pamoja na kumlinda na mabalaa yote.

Msama amesema baada ya kufanya tamasha hilo kwa kishindo Jijini Mwanza sasa ni zamu ya Arusha ambapo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi.

“Rais wetu Maana ana majukumu mengi kama mnavyoona anasafiri anakwenda kila kona lazima Rais wetu tumpende tumweke mikomoni mwa Mungu amlinde.

“Ampe kila kitu anachohitaji ili aweze kutuongoza, tuendeleaa kuwa na amani kama mnavyoona nchi yetu imekuwa na matukio mengi pasipo kumkabidhi mbele ya Mungu matukio yatakuwa yanaendelea,” amesema Msama.

Amesema baada ya kutoka Jiji Arusha Desemba 11 mwaka huu watakuwa Jijini Dodoma na baadae wataelekea Singida na Kahama.

Msama amewataja wasanii watakaoshiriki katika tamasha hilo kuwa ni Rose Muhando,Joshua Mlelwa,Boniface Mwaitege na waimbaji kutoka mataifa mbalimbali huku akidai kiingilio ni bure.

“Nawaambia wakazi wa Mkoa wa Arusha wakae tayari hakutakuwa na kiingilio litakuwa tamasha kubwa na la bure kabisa tunawambia waje kila kona ili kumwombea Rais wetu,”alisema Msama

Kwa upande wake Mratibu wa tamasha hilo, Emmanuel Mabisa amesema katika tamasha hilo Kwaya mbalimbali zitatumbuiza na Maaskofu wa makanisa mbalimbali wamejipanga kutoa neno la Mungu.

“Watumishi wa Mungu wamejipanga maombi yanaendelea tunamuombea Rais kwa sababu ya kazi kubwa anazofanya.Tumeamua kuzunguka tutaendelea kufanya hivi mpaka hali itakapokuwa shwari wakazi wa Arusha waendelee kujiandaa kama Mwanza, ”amesema mratibu huyo.

Chanzo: Mwanaspoti