Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasanii wa Tanzania wametuzidi mashabiki sio kuimba - Chameleone

Jose Chameleone Wasanii wa Tanzania wametuzidi mashabiki sio kuimba - Chameleone

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii Mkongwe wa Muziki, Jose Chameleone amesema licha ya Muziki wa Uganda kuachwa nyuma na Kenya na Tanzania, bado Taifa hilo linajivunia uwezo wa kuimba walionao wasanii wake ambapo hakuna Msanii wa Tanzania wala Kenya anayefikia uwezo huo.

Amekiri, Muziki wa Uganda uliyumba kutokana na wasanii kushindwa gharama akitolewa mfano wakati Kenya ikiwa na Studio 50 Uganda walikuwa na Studio 3 huku #Tanzania Mashabiki waliwachukulia Wasanii wake kama Wafalme.

Nyota huyo wa Ngoma za "Valu Valu" na "Tubonge" ameongeza “Naweza kukwambia hivi, Majirani zetu wametuzidi kwa Vifaa na Upendo wa Mashabiki lakini hawawezi kuimba kama sisi. Hiyo ndio Silaha pekee tuliyonayo na tunapaswa kuwekeza hapo mengine yatakuja"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live