Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasanii wa Konde Gang kusepa mwezi ujao

Harmonize Na Ujumbe Wasanii wa Konde Gang kusepa mwezi ujao

Sun, 25 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Big Boss wa Kond Gang, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ ametanga kuwa kuna baadhi ya memba wake watahitimu katika lebo yake hivyo watakuwa huru kwenda kujitafutia maisha.

Harmonize bila kuwataja majina wasanii hao, ameandika kupitia Insta Story yake kuwa kuna baadhi ya memba watahitimu na atawatangaza siku ambayo anasherehekea miaka mine ya lebo hiyo.

“Tarehe 10/10 kondegan tunatimiza rasmi miaka 4. Sio rahisi asikuambie mtu, vipindi vya kucheka, kulia kuteleza na kuamka yote tunamshukuru Mungu pamoja na wewe unayesoma umefanikisha kuifanya Kondegang kuwa label kubwa Afrika Mashariki asante sana.

“Lengo ni kujikwamua kama watoto wa kimasikini tunatarajia kufanya jambo kubwa jambo kubwa katika siku hiyo kubwa kwetu ikiambatana na kuhitimu kwa baadhi ya members kadhaa wa KondeMusic,” aliandika Harmonize.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live