Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasanii wa Bongo kushiriki matamasha China

RAIS SAMIA WEB Wasanii wa Bongo kushiriki matamasha China

Mon, 27 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wasanii wa Tanzania wa muziki wa Bongo Fleva, Taarab na Vikundi vya Ngoma za Utamaduni watapata fursa ya kushiriki katika Matamasha yatakayofanyika nchini China mwaka 2024 ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Mwaka wa Ushirikiano wa Utamaduni na Utalii kati ya China na Tanzania.

Hatua hiyo ni matokeo ya ziara ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan nchini ambapo Tanzania na China zilikubaliana kwamba mwaka 2024 uwe mwaka wa kukuza Ushirikiano wa Utamaduni na Utalii ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mahusiano ya Kidiplomasia baina ya China na Tanzania.

Taarifa hiyo imetolewa Jijini Beijing katika Mkutano wa Balozi wa Tanzania nchini China Mberwa Kairuki na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China Zhang Weiguo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live