Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasanii kutoka Kenya, Uganda na Nigeria kushiriki katika albamu ya Barnaba

Fri, 26 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki Bongo, Barnaba amesema albamu yake inayotarajiwa kutoka mwishoni mwa February mwaka huu itakutanisha wasanii kutoka Kenya, Uganda na Nigeria.

Muimbaji huyo ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa albamu hiyo itakuwa na nyimbo 15 badala ya nane alizopanga hapo awali.

“Wengi akiwemo Le Band kutoka Kenya, Juliana Kanyomozi kutoka Uganda, Jose Chameleon kutoka Uganda, kwa Bongo hapa kuna msanii kama Vanessa Mdee, G Nako, Ben Paul, Aslay, Barakah The Prince na Linex,” amesema Barnaba.

Ameendelea kwa kusema amefanya kolabo na wasanii wawili kutoka Nigeria ambao hakutaka kuwataja majina kwa sasa, pia alipoulizwa na iwapo ana kolabo na Tiwa Savage hakutaka kuweka wazi hilo.

Chanzo: bongo5.com