Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasanii kupata chanjo ya COVID-19 Karimjee

Yuuii katibu Mkuu wa Wizara ya Habaro, Dkt. Hassan Abbasi

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: millardayo.com

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya imeratibu zoezi la hiari kwa Wadau wa sekta hizo kupatiwa chanjo ya Covid–19.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa makundi hayo yamependekezwa kupewa kipaumbele kwa kuzingatia, pamoja na mambo mengine, umuhimu wao kwa jamii na ukweli kwamba kwa mazingira ya kazi zao wako katika hatari ya kuambukizwa.

“Shime kwao kujitokeza siku ya Alhamisi na Ijumaa wiki hii Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam kuanzia saa tatu asubuhi kwa hiari yao wale waliojiandikisha katika Mabaraza na Idara zao husika”—Dkt. Abbasi

Abbas amesema kwa wale waliokosa kujiandikisha awali wawe Wasanii au Wanahabari au Wanamichezo wajiandikishe mapema kupitia namba 0654063274 au barua pepe [email protected] ya Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Amefafanua kuwa Wasanii walio nje ya Dar es Salaam wataendelea kutumia utaratibu unaoendelea kutangazwa na Wizara ya Afya.

Chanzo: millardayo.com