Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasanii kumsindikiza Magufuli Dodoma leo

1bf872052c200d398b9a5c3467f602ff Wasanii kumsindikiza Magufuli Dodoma leo

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WASANII kibao leo watatumbuiza katika hafla ya kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Msanii nguli wa mashairi Mrisho Mpoto alisema kuwa kundi la wasanii lilioundwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo litatumbuiza wakati wa kuuaga mwili wa Magufuli.

Juzi na jana wasnii kibao walitumbuiza katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam katika siku mbili za kumuaga rais huyo wa Awamu ya Tano wa Tanzania aliyefariki Machi 17, 2021.

Mpoto akizungunzia kuhusu kutunga wimbo wa kumuaga Magufuli yeye bonafsi, alisema hatafanya hivyo kwani kutokana na ukubwa wa msiba, ataungana na wasanii wenzake kutoa nyimbo.

Alisema aliungana na wasanii wengine kuimba wimbo wa Wasafi na sasa ameungana nao kuimba wimbo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa kumuaga Magufuli.

Alisema kuwa wimbo huo wameurekodi kwa produza Kimambo

Chanzo: www.habarileo.co.tz