Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasanii, Watangazaji walivyomzungumzia Ruge Mutahaba

Wed, 27 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Majonzi na simanzi zimetawala nchini Tanzania kufuatilia kifo cha Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kilichotokea leo Jumanne Februari 26, 2019 nchini Afrika Kusini.

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii, watu mbalimbali wamezungumzia kifo hicho  cha Ruge huku wakitumia picha zake na wengine mishumaa.

Msanii barnabaclassic ameandika, “Tazama hapa zmee wewe baba amka. Rugeeeeeeeeeeee jamani moyo wangu mbovu jamaniii baba sitaki amka Mungu wangu jamani baba.Naumia jamani naumia mimi jamani jamani hapana baba si nimekuimbia wimbo jana nikaomba angalau  utumiwe usikie baba sasa baba wee moyo wangu auna nguvu.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Ritha Komba yeye ameandika, “Umeondoka umeacha alama kubwa kwa Taifa, pumzika kwa amani tulio bakia tujiulize tunaacha alama gani kama watoto wa Mungu?.”

“Huu ni muda wa kujiandaa kufanya yaliyo mapenzi ya Mungu na sio mapenzi ya wanadamu dah maisha haya #rip.”

Naye Mr Blue ameandika, “Pumzika kwa amani kaka yetu kipenzi Ruge Mutahaba Mungu kakupenda zaidi $ripruge.”

RY C yeye ameweka picha ya Ruge kisha akaandika, “Asante Ruge huku Ali Kiba akiandika, “R I P UNCLE.”

Aslay Isihaka aliweka picha ya mshamaa na kusema, “Mungu akupe kauli Thabeet Father huko uendapo #RugeMutahaba.” Naye AY ameandika, “Pumzika kwa amani kaka yetu #RugeMutahaba tutakukumbuka kwa mengi uliyoyafanya..poleni sana @cloudsfmtz @cloudstv ndugu jamaa na marafiki.”

Mtangazaji maarufu nchini, Maulid Kitenge ameandika, “Mbabe uliyepambania maisha yako hadi dakika ya mwisho. Inauma sana pumzika kwa amani Ruge Mutahaba. Safari yetu sote lakini umetuacha. Innalilah.”

Muna Love yeye ameandika, “Mungu wetu huwa akosei, umemaliza kazi yako shuja, umeenda kufurahi na Baba. Pole kwa familia na @cloudsfmtz @cloudstv Neema ya Mungu iwatawale katika wakati huu.”

Mhariri wa Clouds Media Group, Joyce Shebe amesema, “Kauli zake zitaishi! Mungu ampumzishe, namshukuru Mungu kwa kunipa nafasi ya kufanya kazi na Ruge tangu nikiwa chuo hadi naajiriwa.”

“Walimu wangu Mshana, Mrutu, Maugo, Sungura nawashukuru sana sababu nilitoa pale chuo na Ruge alini chagua mimi na Clifford Ndimbo kutoka wanafunzi 60 tulio fanya interview, aliamini katika uwezo. Nimejifunza mengi. Na zaidi ni kushukuru Mungu.”

Msanii wa Hip Hop ambaye pia ni mbunge wa Mikumi (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa Jay’ ameandika, “Pumzika Pema Boss Ruge Mutahaba.”

Soma zaidi: Ruge Mutahaba afariki dunia, Rais Magufuli amlilia

Mtangazaji Mboni Masimba ameandika, “Daaaah jirani tangulia tuko nyuma yako Inna lillahi waina ilayhi rajiuun. Pumzika mahali pema shujaa Ruge Mutahaba.”

Baadaye, Mboni  ameandika tena  maelezo marefu akisema, “Kaka, shemeji na jirani yangu Ruge Mutahaba, mimi nakuzungumzia kwa upande wangu, wewe ulikuwa ni mtu mwema sana sana sana.”

“Nakumbuka 31/05/2014 Thembonishow tulipata ajali wakati tunatoka Dodoma na tukampoteza Director/ kaka yetu George Tyson, tumefika Morogoro na mwili wa marehemu Tyson, ulinipigia simu kama 10 hivi nikagoma kuzipokea kutokana na maumivu niliyokuwa nayo kwa wakati ule.”

Mbona aendelea kusema, “Nikamwambia mama yangu Ruge ananipigia simu sana, mama akaniambia pokea umsikilize, Daaaah wewe Ruge wewe nakumbuka haya maneno siku zote baada ya kupokea simu yako nililia kwa uchungu sana Ruge uliniambia;

“Mboni naomba usilie msiba huu ni wetu sote na sita kuacha mwenyewe kwenye hili,” amemnukuu Ruge

Soma zaidi: Nape, Mwigulu, Sugu wamlilia Ruge

Mtangazaji huyo ameendelea kusema, “Daaah wewe mtu wewe ulimuagiza Mh @anthony_mtaka aje kuniona usiku ule ule na ukahakikisha umesimamia usafiri wa kubeba mwili wa marehemu Tyson na Crew yangu nzima kutoka Morogoro mpaka Dar.”

“Na ulishafanya utaratibu mwili uende moja kwa moja kwa Kairuki Hospital, ulinipokea pale Kairuki Hospital na kunipa moyo sana Ruge na hukuwa nyuma ukanisaidia kuhakikisha namrudisha kaka Tyson Kenya.”

“Nini zaidi niseme kwako Ruge, Mungu akupokee kwa mikono miwili kaka Ruge, yaaan msiba wako umenitonyesha msiba wa Tyson, nyie kaka zangu mlale pema peponi.

Naye Msemaji wa Klabu ya Simba, Haja Manara ameandika, “Ooooh niandike nn!!, wenye uwezo wa kuandika watanisaidia!!! Ruge Mutahaba pumzika kaka, rafiki na kiongozi wa watu!!”

“Poleni familia, poleni @cloudstv,@cloudsfmtz, poleni wasanii wote!!! Rest In Peace my Brother

Chanzo: mwananchi.co.tz